Adam Mchomvu amvuta Buravan wa Rwanda 

394
Adam Mchomvu (kushoto) na Yvan Buravan. Picha zote na Faustin Niyigena.

Wakati wa shoo ya Rwanda Fiesta wikiendi iliyopita wilayani Bugesera, msanii Yvan Buravan alipewa ahadi ya kupelekwa Tanzania kwa ajili ya Serengeti Fiesta mwaka huu.

Serengeti Fiesta ni matamasha ya kuzunguka mikoa ya Tanzania Bara ambayo hufanyika kila mwaka na kukutanisha wasanii kibao kutoka ndani na nje ya Tanzania kwa udhamini wa kampuni ya bia ya Serengeti.

Baada ya Yvan Buravan kutumbuiza ngoma zake kama ‘Ni njye nawe’ na ‘Malaika’, mtangazaji wa Clouds FM Adam Mchomvu alitaka kujua msanii ambaye Wanyarwanda wanataka amchukue Serengeti Fiesta mwaka huu.

Adam Mchomvu wa Clouds FM akielezea Watanzania wanavyokula bata

Sauti za watu wengi zilisikika zikilitaja jina la ‘Yvan Buravan’, ambapo Adam Mchomvu alisema bila shaba watamchukua msanii huyo ambaye anafanya vizuri nchini Rwanda.

Buravan akiimba wimbo wake wa Malaika kwa hisia

Ukiacha utangazaji, Adam Mchomvu pia anakuwa ni MC kwenye matamasha ya Serengeti Fiesta yanayoandaliwa na kituo cha habari anachofanyia kazi cha Clouds Media Group.

Buravan akiongea na mashabiki wake kutaka kujua wimbo wanaotaka awachezee

Alipotoa ahadi hiyo alikuwepo Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds, Ruge Mutahaba, ikiwa na maana kwamba yapo matumaini ya Yvan Buravan kupelekwa Tanzania kutanua muziki wake.

Buravan na Uncle Austin wakiimba wimbo walioshirikiana unaoitwa
Mashabiki wa Buravan wakimsikiliza kwa makini wakati anaimba
Wadau wa muziki walikuwa wamejitokeza kwa wingi kwa ajili ya Rwanda Fiesta iliyokutanisha majina makubwa kwenye ramani ya muziki wakiwemo Morgan Heritage kutoka Jamaica

Kutamatisha matamasha ya Serengeti Fiesta wasanii wakubwa kutoka nje ya Tanzania hualikwa, mifano hai ni Rick Ross mwaka 2012 na T.I. mwaka 2014.

Weka maoni