Ajali ya lori la NPD-COTRACO yawaua wanafunzi watatu na dereva Nduba

119
Hivi ndivyo lilivyogeuka lori hilo baada ya ajali

Watu 4 wakiwemo wanafunzi 3 na dereva wa lori wamefariki dunia leo hii kufuatia ajali ya barabarani ambapo lori hilo limewagonga watoto maeneo ya Nduba Jijini Kigali.

Gari hilo aina ya Benz la kampuni ya ujenzi ya NPD-COTRACO lenye namba ya usajili RAD 731J limewaua watoto hao papo hapo ikiwa ni majira ya saa sita za mchana.

Baada ya gari kupinduka, dereva pia alipata majeraha ambapo amewahishwa hospitalini kabla ya umauti kumvuta.

Msemaji wa Jeshi la Polisi kitengo cha Usalama wa Barabarani, CIP Emmanuel Kabanda, amesema lori hilo lilikuwa linatokea Nduba likielekea Gasannze.

Mbali na watoto husika, lori limegonga na nyumba na kuibomoa ila kwa bahati nzuri hakuna mtu aliyekuwemo, kwa mujibu wa maelezo ya CIP Kabanda.

Chanzo cha ajali hiyo hakijajulikana.

Polisi wanasema juhudi za upelelezi zimeanza.

Weka maoni