Akon kurudi Rwanda kwa ajili ya Youth Connekt Africa Summit

273

Kupitia mtandao wa Instagram nguli wa muziki wa Marekani Aliaume Damala Badara ‘Akon Thiam’ anatarajiwa kuja Rwanda kwa ajili ya kikao cha “Youth Connekt Africa Summit” kitakachofanyika tarehe 19 -21 Julai 2017 mjini Kigali.

Msanii huyu wa ngoma za miondoko ya RnB na Hip Hop ana asili ya Senegal. Mwaka 2015 alikuja Rwanda katika juhudi za kutanua mradi wake wa usambazaji umeme.

Kikao cha Youth Connekt Africa Summit kitajumuisha vijana kutoka nchi nyingi za bara la Afrika, na inatarajiwa kuwa Akon atawahutubia kuhusu jinsi ya kujiendeleza kibiashara.

Kikao husika kitawakutanisha wawekezaji zaidi ya 1500 kutoka nchi tofauti.

Rwanda ni mojawapo ya nchi 14 za Afrika ambazo zitanufaika na mradi wa Akon wa kusambaza umeme ambao unawalenga Waafrika zaidi ya miliyoni 600.

Akon ambaye alizaliwa mwaka 1973 alijihakikishia umaarufu wa kimataifa kutokana na nyimbo zake zilizofanya vizuri mathalani Right Now, Beautiful, Ghetto, Be with u, I’ m so Paid na nyinginezo nyingi.

Weka maoni