Ali Kiba kuingiza sokoni bidhaa za nembo yake ‘King Kiba’

674
Ali Kiba

Msanii wa muziki kutoka nchini Tanzania Ali kiba ametangaza ujio wa bidhaa mbalimbali kutoka katika nembo yake ‘AK’ pamoja na ‘King Kiba’.

Muimbaji huyo wa Aje, amesema kuwa hiyo ni mipango mizito na hatarajii kuifanya kiholela kwani hata mwanzo alitoa baadhi ya bidhaa kwa lengo la kuzitangaza.

“AK ni brand ya Alikiba nashukuru imekuwa kubwa watu wanavaa lakini pia ipo na ya King Kiba nayo ni brand yangu na zipo official kabisa na kazi zitakapoanza watapata product zote,” Alikiba alikiambia kipindi cha XXL cha Clouds FM.

Aliongeza, “Kuna malengo makubwa sana tumeyaweka lakini siwezi kusema sasa hivi ila kuna jeans, viatu na glasses tayari zishatoka soon wataziona maana hizi zitakuwa za kwanza sababu tayari zishatoka na kuna energy drink”

Wiki mbili zilizopita muimbaji Diamond Platnumz naye alizindua manukato yake yaitwayo Chibu Perfume.

Chanzo: Bongo5

2 Maoni

  1. Ali Kiba namkubali mno aendelee kufanya maajabu amfunike fala anayejiita Chibu Dangote, mimi #TeamKiba forever

  2. Ali Kiba namkubali mno aendelee kufanya maajabu amfunike fala anayejiita Chibu Dangote, mimi #TeamKiba forever

Weka maoni