Alicia Keys kuja Rwanda mwezi ujao

341

Hatimaye imethibitika kuwa nguli wa muziki kutoka Marekani Alicia Keys atakuja Rwanda mwezi ujao kwa ajili ya Kigali Up Festival.

Mwezi uliopita waandaaji wa tamasha hilo walikuwa hawajawa na uhakika kuhusu ujio wa msanii huyu, ambapo walisema wanaongea naye ila bado hawajafikia mwafaka.

Kipindi hicho waandaaji wa Kigali Up Festival walisema miongoni mwa vipingamizi vilivyokuwepo ni pamoja na uwezo wa kumlipa Alicia Keys.

Hata sasa hivi hawajasema kama walipataje uwezo huo wa kipesa na wala hawajabainisha kama watamlipa kiasi gani, ila wamesema mambo yameshaiva.

Mtoa habari ambaye ni mmoja kati ya wahusika wa uandaaji wa Kigali Up ambaye hakutaka jila lakwe litajwe, amesema mambo yameshanyookakwa hiyo wapenzi wa Alicia Keys na Kigali Up Festival wakae mkao wa kula.

 

Wasanii wengine kutoka nje ya Rwanda ambao watashiriki Kigali Up Festival ni pamoja na

Ismaël Lô hitmaker wa ‘Tajabone’ na ‘Africa’, na Angelique Kidjo ambaye ni msanii mkubwa kwa Afrika kutoka nchini Benin.

Tamasha la Kigali Up linakwenda kufanyika kwa mara ya saba. Safari hii litaanza tarehe 19 Agosti na kumalizika tarehe 19 mwezi huo huo, likiwa limelenga kuwainua wasanii wa kike.

Tamasha kama hilo la mwaka jana lilishuhudiwa na wasanii kutoka nchi mbalimbali wakiwemo Skyler Jett ambaye aliwahi kuwa mshindi wa Grammy Award.

Weka maoni