Alvaro Morata amekamilisha usajili rasmi Chelsea.

206

Mshambuliaji Alvaro Morata amefanikiwa kusaini mkataba rasmi wa kujiunga na Chelsea.

Morata ambaye ametokea Real Madrid ya Hispania amesaini mkataba wa kujiunga na mabingwa hao wa ligi kuu ya Uingereza kwa msimu uliopita kwa mkataba wa miaka mitano.

Hata hivyo dau la uhamisho wa mshambuliaji huyo limekuwa na utata ndani yake huku gazeti la Telegraph likidai mchezaji huyo amesajiliwa kwa paundi milioni 80 huku vyombo vingine vikidai amesajiliwa kwa paundi milioni 70.

Weka maoni