Mchekeshaji mashuhuri Anne Kansiime kurudi Rwanda

161

Mwanamke raia wa Uganda ambaye amejizolea sifa lukuki kutokana na kipaji chake cha kuchekesha, Anne Kansiime anatarajiwa kurudi Rwanda mwezi huu.

Tamasha atakalokuja kushiriki ni lile la ‘Seka Live’ ambapo watakuwepo pia wachekeshaji maarufu nchini Rwanda wa kundi la Comedy Knights.

 

Mmoja wa wahusika wa maandalizi ya tamasha hilo ameiambia Habari Pevu wameshapanga kila kitu na Anne Kansiime na maandalizi ya tamasha yanaelekea ukingoni.

Mara ya mwisho Anne Kansiime kuja Rwanda ilikuwa tarehe 24 Julai 2016 katika ‘Arthur na Kansiime Live, ambapo akishirikiana na mchekeshaji mwenzaje Nkusi Arthur waliwaacha hoi wapenzi wa vichekesho.

Shoo ya ‘Arthur na Kansiime Live’ iliwakamata watu wengi ambao hawakuweza kuficha hisia zao.

Anne Kansime alizaliwa mwaka 1987 maeneo ya Mparo wilayani Kabale Magharibi mwa Uganda.

Baadhi ya magazeti ya Afrika Mashariki humuandika kwa kumuita East Africa’s Queen of Comedy’

 

 

Weka maoni