Arsenal yakubali kichapo kutoka kwa Liverpool EPL

135

Arsenal imekumbana na kipigo cha aibu kwenye Ligi Kuu ya England baada ya kutandikwa 4-0 na Liverpool katika dimba la Anfield. Liverpool waligawa dozi ya bao mbili kwa kila kipindi ambapo  Roberto Firmino alifunga katika dakika ya 17 huku Sadio Mane akitupia la pili dakika ya 40. Kipindi cha pili kikaendelea kuwa kigumu kwa Arsenal pale mshambuliaji mpya Mohamed Salah alipofunga bao la tatu dakika ya 57 kabla Daniel Sturridge hajahitimisha karamu ya magoli dakika ya 77. Ni bao la Salah ndio lililosisimua zaidi pale alipotoka katikati ya uwanja na kuchanja mbuga hadi kwenye 18 ya Arsenal na kumtungua kipa Petr Cech. Mshambuliaji anayegoma kusaini mkataba mpya Arsenal, Alexis Sanchez alicheza kwa mara ya kwanza msimu huu lakini hakuwa na msaada wowote kwa timu yake na kujikuta akipumzishwa dakika ya 62, nafasi yake ikichukuliwa na Olivier Giroud.

Weka maoni