Auddy Kelly kurudi kwenye muziki kwa shinikizo la mashabiki

308

Taarifa zilizotufikia zinathibitisha msanii Auddy Kelly kughairi uamuzi wake wa kuachana na muziki kabisa baada ya kushinikizwa na mashabiki.

Msanii huyo ambaye alijihakikishia umaarufu nchini Rwanda kwa nyimbo zake zilizofanya vizuri kama Sinzagutererana, Ruzakugarura, Ndamutse, Ndakwitegereza, Nkoraho Mana, tarehe 25 Aprili mwaka huu alitangaza kuacha muziki.

Kipindi hicho Auddy Kelly alitangaza uamuzi wake wa kuachana na shughuli zote za muziki kupitia kurasa zake za Facebook na Intagram ambapo aliandika hivi: (nimetafsiri kwenda Kiswahili)

“Habari yenu ndugu zangu, nimekuwa nikifikiria kuhusu uamuzi huu kwa miezi mitatu. Ndiyo maana kwanza natanguliza kuwaomba msamaha watangazaji walionialika kwenye vipindi vyao nikawa naomba tuahirishwe, hakuna msanii anayepiga deki bahati kama hiyo ila nimeshachukua uamuzi huo mgumu wa kuacha muziki, naomba kauli yangu isichukuliwe vibaya kusema kweli nawaheshimu wote.”

https://www.youtube.com/watch?v=9z_L8BZZf-w

Baada ya tangazo hilo mashabiki wake waliendelea kumuonesha ni jinsi gani wamechukizwa na uamuzi wake, ambapo walisema waliona anaweza muziki kwa hiyo anatakiwa aendelee kuwepo kwenye gemu kwani wanapenda kazi zake.

Hapo jana Jumapili msanii huyu alikutana na kuzungumza na wawakilishi wa kundi la mashabiki wake liitwalo “La Familia” ambapo walikubaliana kwamba ana sababu nyingi za yeye kurudi kwenye ulingo wa muziki.

Baada ya mazungumzo hayo, kupitia mitandao ya Facebook na Instagram Auddy Kelly alitangaza kurudi rasmi kwenye ramani ya muziki.

Ameandika, “Natumai hamjambo. La Familia mna nguvu sana mmefanya nibadili baadhi ya maamuzi yangu, niko tayari kurudi ila si mwaka huu bali ni mwaka ujao. Isingekuwa nyinyi ningepotea kabisa kwenye ramani ya muziki na kubaki naimba sebuleni kwangu na bafuni tu…”

Auddy Kelly amemalizia ujumbe wake kwa kusema kuwa anashukuru waandishi wa habari kwa kumpa uungaji mkono wao katika kila jambo alilofanya.

Weka maoni