Waandishi Zilizoandikwa na Jalilu Zaid

Jalilu Zaid

115 Habari 0 Maoni
Blogger |Sports Analyst |Photographer |Radio Presenter. A true definition of hustler.

Rick Ross na Briana Camille wapata mtoto wa kike

Rapper kutoka Maybach Music Group(MMG), Rick Ross amebahatika kupata mtoto wake wa kwanza na mwanamitindo Briana Camille. Licha ya kuwa wawili hao hawakuwahi kutangaza kuwa katika mahusiano ya kimapenzi na wala hawakuwahi kuonekana pamoja ila wamebahatika kupata mtoto wa kike. Inaelezwa kuwa Camille alikuwa akimsapoti...

Klabu ya Simba kuanza kuneemeka kupitia Pesa za Mitandaoni.

Kati ya klabu za Tanzania ambazo kwa siku za usoni huenda zikajivunia uwepo na ukuaji wa teknolojia, ni klabu ya Simba.Klabu hiyo kongwe, ambayo umaarufu wake ulianza mwaka 1936, huku ikiwa na wapenzi na mashabiki ndani na nje ya nchi, ina kila dalili ya...

Shirikisho la soka Tanzania kuja na ligi ndogo ya wanawake

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania ‘TFF’, limeagiza Makatibu wa vyama vya Mikoa kutuma haraka majina ya timu mabingwa wa mikoa wa soka la wanawake wa msimu wa 2016/17. Viongozi wa mikoa wamekumbushwa kutuma timu ili kufanya maandilizi ya haraka ya ili kufanyika kwa ligi...

Polisi Rwanda wamshikilia Diane Rwigara pamoja na mama na dada yake

Polisi nchini Rwanda wamesema wanamzuilia mwanasiasa wa upinzani Diane Rwigara, mamake na dadake. Wiki iliyopita polisi walikuwa wametangaza kuwa mwanasiasa huyo anatuhumiwa kughushi nyaraka wakati alipotaka kuwania urais mapema mwezi wa 8 huku familia yake ikituhumiwa kukwepa kulipa kodi. Kwa mujibu wa walioshuhudia, polisi wapatao 10...

Polisi 92 walazwa hospitali wakihofiwa kuugua kipindupindu

Maafisa 92 wa polisi nchini Kenya wamelazwa hospitalini Nairobi na viunga vyake wakihofiwa kuugua ugonjwa wa kipindupindu, wizara ya afya nchini humo imesema. Maafisa hao wamelazwa katika hospitali ya taifa ya Kenyatta, hospitali ya Sinai na katika hospitali ya wanawake ya Nairobi Women’s. “Polisi hao inashukiwa...

Wapinzani Tanzania waanza na mgomo Bungeni

Wabunge wa Kambi ya Upinzani Bungeni wamesusia kuapishwa kwa wabunge saba Viti Maalumu wa Chama cha Wananchi (CUF) katika mkutano wa nane Bunge la 11 kwa madai hawakufurahishwa na maamuzi ya kufukuzwa wabunge 8 wa Viti Maalumu wa chama hicho. Mkutano wa nane wa Bunge...

Azam FC yatunukiwa na shirikisho la soka TFF

Klabu bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, imeishukuru Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa kusema wanaishukuru kwa kuweza kuwapa haki zao ambayo waliyokuwa wanayostahili kwa kipindi kirefu. Hayo yameelezwa na taarifa iliyotolewa na uongozi wa timu hiyo kupitia ukurasa wao maalum...

Tarehe ya kurudia uchaguzi nchini Kenya yatajwa rasmi

Baada ya Mahakama ya juu kufuta matokeo ya uchaguzi nchini Kenya, hatimae Tume ya Taifa ya uchaguzi nchini humo (IEBC), imetangaza tarehe mpya ya kurudia uchaguzi huo. uchaguzi mpya wa urais nchini humo utafanyika tarehe 17 Oktoba mwaka huu. Mwenyekiti wa tume hiyo, Wafula Chebukati...

Alex Oxlade-Chamberlain amefanikiwa kujiunga na Liverpool

Hatimaye aliyekuwa mchezaji wa Arsenal, Alex Oxlade-Chamberlain amefanikiwa kusaini mkataba wa kujiunga na Liverpool. Mchezaji huyo amejiunga na Majogoo hao wa Anfield kwa ada ya uhamisho wa paundi milioni 40. Awali Chamberlain alikuwa akiwaniwa kwa ukaribu na Chelsea ambayo hakufanikiwa kuipata saini yake. Hata hivyo mchezaji huyo...

Klabu ya Simba kumpandisha kizimbani mchezaji wake

Uongozi wa klabu ya Simba kupitia Afisa habari wake, Haji Manara wamesema wamedhamiria kumpeleka Mahakamani Kiungo Pius Buswita ambaye alisaini baada ya kutoa Lugha za uchochezi dhidi ya Klabu hiyo. Manara amebainisha hayo baada ya kusikia maneno yasiyo ya kiungwana yakisemwa na mchezaji huyo kwa...