Baada ya Wema Sepetu, hata TID ampa makavu Harmorapa

501

TIP ambaye kwa sasa anapenda kuitwa jina la Mnyama, amesema Harmo ni msanii ambaye hajui muziki lakini anataka kuimba.

“Harmorapa ni mtu asiyejua muziki lakini anataka kuimba,” TID amekiambia kipindi cha On The Eight cha TVE.

Hata hivyo sio muimbaji huyo pekee ambaye ameonekana kutomkubali rapper huyo, wengine ni Master J, Afande Sele na wengine, kwa mujibu wa Bongo5.

Harmorapa juzijuzi alipewa makavu pia na Wema Sepetu ambapo Wema alisema hawezi kuwa mpenzi wake, ikiwa ni baada ya Harmorapa kudai kuwa anamtamani Wema kimapenzi.

Wema alimtaka Harmo asimharibie jina na asiendelee kumtaja kwenye vitu vyake na kumuomba amheshimu kama msanii mwenzake akome kumuongelea.

Sikiliza hapo chini Wema alivyomchomolea Harmorapa.

Sikiliza huu wimbo ‘Kiboko ya mabishoo’ wa Harmorapa na Juma nature akikuambia “tulikuwa wasafi kabla ya WCB” na “maneno yao machafu hayanivunjii CV”

Weka maoni