Baba yake na Belle 9 afariki dunia kwa kugongwa na boda boda

177
Belle 9, mmoja kati ya wasanii wazuri wa Bongo Fleva

Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka Tanzania Abedinego Damian aka Belle 9 amefiwa na baba ambapo baba yake amefariki kwa kugongwa na bodaboda usiku wa tarehe  Aprili17, 2017.

Jahz Zamba ambaye ni meneja wa Belle 9 ameiambia Bongo5 kuwa Mzee Damian alivunja mguu mmoja pale pale na kujeruhiwa vibaya kabla ya kupelekwa hospitali.

Katika ajali hiyo dereva wa pikipiki amevunjika taya na kujeruhiwa kichwa. Mzee Damian aliwahishwa hospitali akiwa mahtuti ambapo muda si mrefu alifariki dunia.

Amefariki ikiwa ni baada ya kaka yake Belle anayeishi Morogoro kwenda kuzisaka dawa ambazo zilikuwa zimekosekana hospitalini.

Hili ni pigo kwa Belle 9 ambaye ‘Sumu ya Penzi’ na ‘Masogange’ ni miongoni mwa nyimbo zilizomzolea umaarufu kwa kuwa mara nyingi hudai baba yake ni mwalimu muhimu katika maisha yake.

“Mfano hai ni kwamba mpaka leo hii hapa, baba yangu bado yupo na mama yangu ni kitu ambacho nakuwaga proud,” alisema kwenye kipindi cha Ngaz Kwa Ngaz cha Salama Jabir.

“Ninavyorudi nyumbani, baba yupo, mama yupo sababu nina rafiki zangu wengi ambao wako na mama zao peke yao wengine wako na baba zao peke yao, so kwangu mimi baba yangu ni mwalimu katika hilo,” aliongeza.

Pia Belle aliwahi kukiambia kipindi cha The Playlist cha Times FM kuwa couple anayoikubali zaidi ni ya wazazi wake. “Baba yangu na mama yangu,” alijibu muimbaji huyo.

“Wananivutia kwasababu nyumbani maisha ni ya kawaida lakini still baba yuko na mama halafu mara zote ambazo nimekuwa nyumbani, sijawahi kuona mama yangu anagombana na baba. Mimi nimekaa sana nyumbani kwa muda mrefu, lakini mara ya kwanza naona kama wanashikanashikana hivi ilikuwa mimi ndio chanzo, yaani mama alikuwa ananitetea mimi kwa sababu baba alikuwa ananinyoosha sana sasa mama alikuwa kama anaingia hivi, lakini haukuwa ugomvi,” aliongeza.

“Kiukwezi ni best couple kwangu mimi, najifunza mengi kupitia pale, inanipa nguvu nikirudi nyumbani baba yupo, mama yupo nikitoka hapo nami nakuwa nipo fast kila kitu.”

Weka maoni