Bac T adondosha wimbo mpya wa Dancehall uitwao Tell me

107
Bac T

Msanii wa Rwanda Nkubiri Gerard almaarufu Bac T ambaye pia ni mtangazaji wa Family TV, jumatatu wiki hii alidondosha wimbo wake mpya wa Tell me.

“Tell me ni wimbo ulioko katika miondoko ya Dancehall. Tofauti na watu wanavyonijua kama mimi ni msanii wa Hip Hop ila pia ni mkali wa miondoko ya Dancehall,”amesema Bac T.

Akizungumzia maudhui ya wimbo huo, Bac T amesema ni wimbo wa mapenzi aliomuimbia mpenzi wake ampendaye kwa dhati.

“Namuambia mpenzi wangu aniambie chochote anachotaka ili nimfanyie kwa sababu nampenda sana basi hakuna kitu anaweza kukosa kwangu,” amesema katika mahojiano na Habari Pevu.

Hii ni moja kati ya ngoma zitakazokuwa kwenye albamu yake itakayoitwa Dancing Station na ndio wimbo wake wa kwanza kutoka mwaka huu.

Tell me imetengenezwa ndani ya studio za Kigali Records na mzalishaji Lil Pro.

Bac T amekuwa akifanya muziki na utangazaji pia kwa muda mrefu, na miongoni mwa ngoma zilizoinua jina lake kwenye ulingo wa muziki wa Rwanda ni pamoja na ‘Nimuamini nani’ na More Fire aliyoshirikiana na kundi la TMK kutoka Tanzania.

Msanii na mtangazaji wa Family TV, Bac T

Weka maoni