Bajeti ya kilimo inaweza ikapungua kwa asilimia 30

192

Wizara ya Fedha na Mipango nchini Rwanda (MINECOFIN) imeliambia bunge kuwa bajeti iliyotengwa kwa ajili ya kilimo itapungua kutoka bilioni 118 hadi kufika bilioni 80.

Hatua ya kupunguza bajeti hiyo kwa kiwango cha asilimia 30 kutoka bilioni 118 hadi kufika bilioni 80 imewashtua wabunge waliohoji misingi yake.

MINECOFIN imetoa tamko hilo wakati ikifafanulia wabunge ambavyo baadhi ya miradi itakavyotumika.

Katibu wa Kudumu katika Wizara ya Fedha na Mipango, Celeb Rwamuganza, akiongea na Redio Rwanda, amesema kuwa mojawapo ya sababu za kupunguzwa kwa bajeti ya kilimo ni pamoja na kuwa kuna baadhi ya miradi ya kilimo ambayo hivi sasa iko ukingoni kumalizika.

Celeb ametoa mfano ya mradi wa kunyunyizia mazao na kusema unakaribia kukamilishwa, uko lakini wanasubiri miradi mingine kutoka nchi za nje.

Aidha Bwana Celeb ameongeza kuwa pesa zilizotengwa hazikupungua kwani hata wanapoongeza bajeti hujikita katika wizara ya kilimo.

Wabunge wameambiwa kuwa utekelezaji wa miradi kwa mwaka huu hivi sasa umefika katika asilimia 70% huku yakiwepo matumaini ya kufikia asilimia 90 mwishoni mwa mwaka huu.

Nchini Rwanda kilimo kina manufaa mengi kwa uchumi wa taifa kwani Wanyarwanda wapatao 70% ni wakulima.

Rwanda ina kilometa za mraba zinazotumiwa kwa ajiliya kilimo zipatazo hekari elfu 45, wakati ambapo kunatarajiwa kunyunyuzia mazao hekari 100 mwaka 2020.

Weka maoni