Barcelona yakubali kichapo kutoka Real Madrid

108

Timu ya Real Madrid imeichapa Barcelona kwa mabao 3-1 na kujiweka katika nafasi nzuri ya kubeba ubingwa wa Kombe la Super Cup la Hispania, mechi iliyopigwa usiku wa kuamkia leo katika uwanja wa Camp Nou jijini Barcelona.

Mchezo ulionekana mgumu kwa pande zote mbili huku watu wakitaka kuona Barca watakuwaje bila Neymar na dakika ya 50, mlinzi wa Barca Gerrard Pique aliipatia Madrid bao la kuongoza baada ya kujifunga.

Dakika ya 77 Lioneil Messi aliipatia Barca bao la kusawazisha kwa mkwaju wa penati lakini dakika ya 80 Ronaldo aliipatia Madrid bao la 2 kabla ya dakika ya 82 kupewa kadi nyekundu na dakika ya 90 Asensio aliiandikia Madrid bao la 3.

Kwa upande mwingine, timu hizo zinatarajiwa kukutana tena Agosti 17 mwaka huu katika uwanja wa Santiago Bernabeu ili kuweza kuamua nani ataibuka kuwa bingwa.

Weka maoni