Barcelona yathibitisha kuondoka kwa Neymar Jr

380

Klabu ya Barcelona ya nchini Hispania imethibitisha kuwa nyota wake,Neymar ameutaarifu uongozi kuhusu dhamira yake ya kuondoka klabuni hapo.

Barcelona imewataarifu matajiri wa Ufaransa klabu ya Paris St-Germain kuwa ni lazima itoe Euro milioni 222, sawa na pauni milioni 198 kabla ya Neymar kujiunga na timu hiyo kiasi ambacho kitakuwa kimevunja rekodi ya dunia.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazili amewasili katika mazoezi ya timu yake leo Jumatano huku akiwa na Baba yake mzazi pamoja na wakala wake, Wagner Ribeiro na kuuwambia uongozi wa klabu kuwa sasa anahitaji kuondoka

Meneja wa kikosi cha Barca, Ernesto Valverde amempatia ruksa ya kutoshiriki mazoezi

Habari zilizoenea siku za hivi karibu ni klabu hiyo ya Hispania Barca kuhimiza kufanyika kwa uchunguzi wakishinikiza kuwa huwenda Neymar ameshasaini PSG

Neymar  amejiunga na Barcelona akitokea Brazili katika klabu ya Santos mwaka  2013  kwa dau la pauni milioni 48.6 na kusaini kandarasi ya miaka mitano na kuifungia jumla ya mabao 105 huku akiisaidia kuctwaa mataji ya ligi, Copas del Rey na klabu bingwa.

Weka maoni