Benki ya Dunia kudhamini ujenzi wa barabara Ngoma-Bugesera-Nyanza

358
Mwakilishi wa Benki ya Dunia nchini rwanda Yasser el Gammal akibadilishana nyaraka na Waziri wa Fedha na Mipango Balozi Gatete Claver baada ya kumwagia wino makubaliano ya mkopo wa ujenzi wa barabara hiyo

Benki ya Dunia imeiahidi Serikali ya Rwanda mkopo wa faranga miliyoni 70 zitakazotumika kujenga barabara ya kuunganisha wilaya za Ngoma-Bugesera-Nyanza nchini Rwanda.

Ujenzi wa barabara hiyo ya lami unaonekana kama mkombozi wa msongamano wa magari unaoshuhudiwa katika barabara ya Rusumo-Kigali-Huye na ile ya Rusumo-Kigali-DR Congo.

Mwakilishi wa Benki ya Dunia nchini Rwanda, Yasser El-Gammal na Waziri wa Fedha na Mipango, Balozi Gatete Claver wamesaini makubaliano ya mkopo huo leo hii mjini Kigali.

Baada ya kusaini makubaliano hayo, Balozi Gatete Claver amesema “sehemu moja ya pesa ya ujenzi wa barabara hiyo itatolewa na Benki ya Dunia huku sehemu nyingine ikitolewa na Serikali ya Ujapani.”

“Barabara hiyo ina jumla ya kilomita 119 lakini kilomita 66 tu ndizo zitakazojengwa kwa pesa hiyo itakayotolewa na Benki ya Dunia sehemu nyingine ndiyo itolewe na Ujapani.”

Balozi Gatete amesema sehemu ya barabara itayayojengwa kwa mkopo wa Benki ya Dunia itaanzia sehemu inayoitwa Kibugabuga wilayani Bugesera hadi Gasoro wilayani Nyanza Kusini, katika Mkoa wa Kusini.

Balozi Gatete na Yasser wakimsikiliza Waziri anayehusika na masuala ya uchukuzi Dkt Alexis Nzahabwanimana

Mwakilishi mkazi wa taasisi hiyo ya kimataifa nchini Rwanda, Yasser El-Gammal amesema barabara hiyo ikikamilika itawanufaisha raia laki tano.

“Barabara husika itasaidia kuweka mazingira ya uundaji wa ajira kwa wakazi wa maeneo jirani, wengine watapata vibarua katika ujenzi wake…,” ameongeza Yasser.

Aidha, Balozi Gatete amesema barabara hiyo itarahisisha matumizi ya uwanja wa ndege wa Bugesera ambao ujenzi wake umeshaanza, hasa kwa watu wanaotokea maeneo ya Mkoa wa Kusini.

Barabara hiyo ni moja ya ahadi za Rais Dk. John Magufuli kwa wananchi.

Weka maoni