Bill Gates aja nchini Tanzania akutana na Rais Magufuli leo

259

Mfanyabiashara maarufu na tajiri namba moja Duniani, Bill Gates yupo nchini Tanzania kutembelea miradi mbalimbali ya afya ikiwemo mradi wa matumizi ya dawa za matende na mabusha.

Bill Gates jana mapema alikuwa mkoani Tanga na kutembelea baadhi ya vituo vya afya mkoani humo na kuonana na baadhi ya viongozi wanaosimamia miradi hiyo.

Bilionea huyo ameshafika jijini Dar es salaam na leo imeripotiwa kuwa leo amefanya mazungumzo na Rais Magufuli lakini haijajulikana wamezungumza nini.

Weka maoni