Bingwa wa riadha Usain Bolt ashindwa na mmarekani huko London

120

Bingwa wa riadha duniani Usain Bolt amejikuta akidhalilishwa katika mashindano ya riadha ya dunia yaliyoandaliwa na IAAF mjini London.Katika mashindandano hayo ya mita 100 Bolt ameangukia pua kwa kushindwa mbele ya Justin Gatlin ambaye aliwahi kuingia katika kashfa ya matumizi ya madawa yaliyokatazwa michezoni kutoka Marekani ameshika nafasi ya kwanza.

Bolt ameshika nafasi ya tatu katika mashindano hayo wakati Christian Coleman akishika nafasi ya pili. Mashindano hayo ndio yalikuwa ya mwisho kwa Bolt ambapo japo hajafanya vizuri katika michezo hiyo lakini mashabiki wameonekana kumshangilia kwa nguvu zaidi wakati wa kumuaga.

Weka maoni