Video: Diamond aelezea siri ya mafanikio yake, atoa mawaidha kwa vijana

871
Diamond Platnumz

Nyota ya Afrika Mashariki Diamond Platnumz amezungumzia mambo mengi yahusuyo maisha yake kama msanii na maisha yake binafsi ikiwemo mtoto wake wa kike Tiffah na mkewe Zari Hassan.

Siki chache kabla ya kutumbuiza Korogo Festival mjini Nairobi mwishoni mwa mwezi uliopita, Diamond alihojiwa katika Chuo Kikuu cha Nairobi, ambapo alitoa majibu kuhusu masuala mbalimbali.

Anamiliki Lebo ya wasafi Classic Baby ambayo imeyakutanisha majina makubwa kwenye ramani ya muziki si wa Tanzania tu bali Afrika Mashariki kwa ujumla.

“Ukiwa msanii usifanye vitu vibaya au vitu vya kuipoteza jamii, tutumie usanii katika njia nzuri ndiyo maana huwa nafungua record lebel iliyo na wasanii kama Ray Vanny, Harmonize, Rich Mavoko, Queen Darleen na last week nilizindua msanii mpya Lavalava,” amesema Diamond.

“Siwezi kusema eti nina uwezo mkubwa wa kifedha au eti nina akili sana lakini sapoti ambayo napewa na watu ndiyo imenifanya niweze kufikia hapa, na siku zote huwa nasema WCB siyo ya Diamond, ni ya vijana ambao wanataka kufikia kwenye malengo na maendeleo na ndiyo maana najitahidi kuwachukua vijana katika mtaa nao waoneshe talent yao Mungu akiwasaidia wafike mbali kwa sababu naamini nisingesaidiwa nisingefika hapa ndiyo maana namsaidia kila mtu.”

Aidha, Abdul Naseeb almaarufu Simba au Diamond Platnumz, amesema katika maisha yake anahakikisha anawasaidia watu kwa kuwa hajui kesho yake itakuwaje kwani unayemdharau leo unaweza ukawa ndo unamtegemea kesho.

Alipoulizwa kama angependa watoto wake wawe wasanii, amesema anapenda mtoto wa kiume awe msanii na si wa kike (Tiffah) kwa misingi kwamba wasanii wa kike hukutana na vikwazo vingi katika maisha yao ya sanaa ikiwemo kutongozwa.

Diamond na mtoto wake wa kike Tiffah Dangote

Pia Diamond aligusia suala la umuhimu wa akiba maishani, ambapo amesema kila binadamu ambaye ana akili timamu kwenye kichwa chake anatakiwa aiogope kesho kwani usipoiogopa kesho utazitapanya mali zako na mwisho wa siku familia yako itataabika.

Amewataka vijana wawe na moyo wa kujituma na kujiongeza, ambapo alisema yeye aliishia form 4 lakini kwa sasa ana wafanyakazi 51 wanaomsaidia kuweka sawa baadhi ya vitu ambayo hajavisomea yeye.

Amesema ubunifu ndiyo siri ya mafanikio katika maisha ya mwanadamu na mwanadamu ambaye hata ubunifu ataishi maisha mabaya hata kama ana digrii nyingi vipi.

Angalia video hii hapa chini kwa maelezo zaidi na uweze kujua ambacho amekiongea kuhusu Ali Kiba, mkewe Zari na mambo mengine kibao.

Weka maoni