Diamond Platinumz azindua manukato Tanzania

171
Msanii wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz

Mwanamuziki mashuhuri nchini Tanzania Diamond Platinumz amepiga hatua nyingine baada ya kujitosa katika biashara ya uuzaji wa manukato.

Manukato ya mwanamuziki huyo yamepewa jina Chibu Perfume, kwa kufuata jina lake ya utani la Chibu Dangote.

Chupa ya manukato hayo inauzwa takriban Sh105,000 za Tanzania, kwa mujibu wa BBC.

Diamond anaonekana kuwafuata wasanii wengine mashuhuri duniani ambao wamejiingiza katika biashara ya manukato na hutumia umaarufu wa nembo zao kujipatia mapato zaidi.

Mwishoni mwa wiki iliyopita Diamond alikutana na waandishi wa habari kuzindua rasmi bidhaa hiyo ambapo amesema itaanza kupatikana karibia mikoa yote ya Tanzania, kwa mujibu wa Dizzim Online.

Baada ya meneja wa Diamond Platnumz, Sallam SK kutangaza manukato yatakavyouzwa kwenye maduka, baadhi ya watu wamesema kuwa bei hiyo ni kubwa sana.

Hapa Diamond Platnumz ameyajibu yote kuhusu wanaosema kuwa Chibu Perfume ina bei sana, katika mazungumzo ya AyoTV

Kama hukufuatilia manukato hayo yalivyozinduliwa, angalia video hii hapa chini

Weka maoni