Diamond Platnumz aiteka Nyamata kwa masaa mawili (Picha+Video)

1379
Hawa ni wasichana waliopanda jukwaani kuthibitisha jinsi walivyo mahiri katika kumwaga mauno kuliko wasichana wa kikongo

Usiku uliopita ulikuwa ni usiku wa shangwe na furaha tele kwa wapenzi wa muziki nchini Rwanda ambao walikuwa wamefurika kutoka huku na kule kwa ajili ya tamasha la Rwanda Fiesta.

Diamond Platnumz kutoka nchini Tanzania ndiye aliyekuwa msanii wa mwisho jukwaani, ambapo alitumbuiza kwa muda wa masaa yasiyopungua mawili kuanzia saa saba za usiku.

Aliimba muziki wa ‘live’ na ‘semi-live’ ambao mashabiki wake walionekana kuupenda kiasi cha wasichana saba kati yao kupanda jukwaani kumuonesha ni jinsi gani wanajua kucheza.

Akisaidiwa na madensa wanne, aliimba nyimbo zake takribani zote ikiwemo Number One, Nitarejea, Nitampata wapi, Utanipenda, Mawazo, Moyo wangu, Chacun pour soi na kadhalika.

Siku moja kabla ya shoo ya jana aliwatumbuiza wakazi wa mji wa Goma Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ambapo alisema alipenda wanavyokatika na muziki.

Aliwaambia wasichana wa Rwanda kuwa anahisi hawajiamini na hata hahawezi kucheza kama wale wa Kongo, hapo ndipo baadhi yao wakaitwa jukwaani kumthibitishia umahiri wo katika kumwaga mauno.

Baada ya kucheza nao, mmoja wao alimkubatia Diamond kwa hisia na kumpa mabusu mengi huku mashabiki waliokuwa wakishuhudia wakipiga kelele za furaha.

Tamasha la Rwanda Fiesta liliandaliwa na chombo cha habari cha Clouds TV Rwanda.

Wasanii wengine waliokuwepo ni pamoja na Morgan Heritage, Dj Pius, Yvan Buravan, Charly na Nina, Vanessa Mdee na Chege.

Wasichana wakicheza wimbo wa Diamond kwa furaha kubwa
Wasichana saba wa kinyarwanda wakikatika na muziki

Kijana akitumia zana ya muziki kuhakikisha tamasha linanoga
Mashabiki wakitabasamu na kupiga picha wakati Diamond anaendelea na makamuzi yake jukwaani
Msichana huyu alimkumbatia Diamond kwa hisia baada ya kumpa mabusu
Msichana mmoja aliposhindwa kuendelea kuficha hisia zake alimrukia Diamond na kumpa mabusu kedekede

Katika dakika za mwisho mwisho Diamond alivua shati
Hawa ni wasichana waliopanda jukwaani kuthibitisha jinsi walivyo mahiri katika kumwaga mauno kuliko wasichana wa kikongo
Haijulikani hapa Diamond alikuwa anafikiria nini wakati anacheki zigo
Diamond stejini
Diamond akitumbuiza Rwanda Fiesta usiku wa kuamkia leo
Diamond akifanya juu chini kuhakikisha wapenzi wa muziki wake wanafurahi

Diamond akiongea na waandishi wa habari baada ya shoo kumalizika

Picha zote zilichukuliwa na Faustin Niyigena.

Weka maoni