Edsha afungukia penzi lake na Marina: Uncle Austin na The Ben ndio waliliharibu

752
Kutoka kushoto: Edsha, Unche Austin, Marina na thye Ben

Baada ya miaka miwili wakiwa kwenye mahusiano ya kimapenzi, Edsha na Marina majuzi kila mmoja alichukua hamsini zake. “Uncle Austin na The Ben walihusika sana,” kwa mujibu wa Edsha.

Edsha ametaarifu kuwa penzi lake na msanii mwenzake Marina liliingia doa tangu shughuli za sanaa za Marina zianze kusimamiwa na Uncle Austin ambaye hakupenda wawili hao waendelee kupeana vitamu.

“Alitaka kumeneji muziki na mapenzi yetu pia. Awali penzi langu na Marina lilikuwa wazi na kila mtu alijua sisi ni wapenzi, tuliwekana picha zetu kwenye profile Whatsapp na Instagram, Austin alipokuja ndio akaanza kumuambia eti kuweka picha yangu kwenye profile yake italeta madhara,” amesema Edsha katika mahojiano na Habari Pevu.

“Ilipotokea nifarakane kimapenzi na Marina Austin alifurahi sana japo baadaye tulirudiana, akawa anamtaka aachane nami, Marina akawa ananiambia kila kitu mpaka nina screenshots za jumbe zao kuhusu mimi, siku nyingine alipoweka picha yangu tena ya kawaida kwenye profile yake jamaa alimkaripia sana eti nilikukataza kufanya hivyo, eti hizo picha za wanaume kwenye profile yako zitakugharimu…”

Pamoja na kwamba Edsha ametuonyesha jumbe hizo za Whatsapp kati ya Marina na Uncle Austin, lakini wawili hao wamiyatupilia mbali madai yake wakisema hayana ukweli wowote.

“Inawezekanaje mtu awe na tatizo na mtu ambaye hata hawafahamiani? Edsha na Austin hawafahamiani. Austin hajanikataza kumposti Edsha. Austin hajahusika hata kidogo na mimi kuachana na Edsha,” amesema Marina akizungumza na Habari Pevu.

Austin ambaye ananyooshewa kidole akitajwa kuwa yeye ndiye chanzo cha kuvurugika kwa penzi la wawili hao mpaka kufikia hatua ya wawo kumwagana, amesema anameneji muziki wa Marina na siyo mapenzi yake.

“Mungu wangu! Hata sikujua msichana huyo ana mpenzi. Jamaa anatafuta kiki ila angetafuta kiki za kueleweka na siyo kunisingizia. Sikujua ni wapenzi mpaka juzijuzi walipoposti picha inayowaonesha wakibusiana. Huyo Edsha simfahamu nitamkatazaje sasa kupendana na mtu ambaye hata kumfahamu simfahamu? Kuposti picha ya mpenzi wake au kutoposti ni uamuzi wake mimi sihusiki,” amesema Uncle Austin ambaye ukiacha kusimamia kazi za Marina ni mtangazaji wa Kiss FM na msanii wa Afro Beat pia.

Aidha rapa huyo amesema hata jumbe za Whatsapp ambazo msanii The Ben alikuwa akimtumia Marina zilifanya penzi lao lianze kuyumba. The Ben ni msanii mkali wa RnB naye kutoka nchini Rwanda.

Mwishoni mwa mwaka jana ndipo The Ben aliporudi nchini Rwanda kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka sita. “Aliporudi ndipo akaanza mawasiliano na Marina ambapo walipanga kufanya wimbo wa kushirikiana” amesema Edsha.

Katika hatua nyingine Edsha amesema The Ben na Marina walipiga picha ambazo zimekaa kimapenzi zaidi ambazo “ilibidi tuzifute.”

“Aliporudi Marekani waliendelea kuwasiliana ambapo The Ben alikuwa anamuita Mon Coeur (Moyo wangu) ikanifanya nimuulize Marina kulikoni, kaniambia tunashauriana mambo ya muziki tu hatutongozani, ila cha kustaajabisha The Ben akawa anampigia simu mara kama tano kwa siku. Tulipomalizana juzijuzi alifuta picha yangu Instagram na kuweka video akimuambia maneno matamu The Ben, iliniuma sana…”

Alipoulizwa kama aliwahi kuongea na Uncle Austin na The Ben kuhusu kilichotokea, amesema hajawahi kufanya hivyo kwani “sina wivu uliopitiliza”.

“Kilichonikera zaidi, kama siku moja baada ya mapenzi yetu kuisha kuna kundi la Whatsapp ambalo mimi na yeye tulikuwemo alidumbukiza picha ya The Ben akimpa busu la shavu,” ameongeza Edsha.

Jitihada za kumtafuta The Ben ili atupe kauli yake kuhusu madai haya ya Edsha hazijafua dafu. Tukimpata tutawajulisha atakachotuambia.

Wazo moja

  1. Edsha baramukoranye nyine nonese Austin yibutse ko kumanajinga bibaho ari uko abonye Marina? ubundi se araba atarabasha kugeza umuziki we ahakwiye amanajinge abandi ubwo azabivamo? Uyu mukobnwa nawe ndabona aje nabi nonese aratandukana na Edsha akajya kwa Austin at the same time agacudika na Nizzo ubundi akohererezanya amabizu na The Ben ubwo bizavamo? Iby’abahanzi bacu birandangiza ndabarahiye, gusa Edsha nawe gabanya gushyira hanze ibyo waganiraga na Marina si byiza kumuteza abantu kora ibihangano byiza uve mu bugambo

Weka maoni