Erasto Nyoni aibeba Simba huko Afrika Kusini

302

Mchezaji kiraka, Erasto Nyoni ambaye amesajiliwa klabu ya Simba akitokea Azam FC ameibeba Simba Afrika Kusini baada ya kuipatia goli moja timu yake dhidi ya Bidvest ya Afrika Kusini katika mchezo ambao umekwisha kwa timu hizo kutoka sare ya 1-1.

Simba ilicheza mchezo wa pili wa kirafiki ikiwa nchini Afrika Kusini katika maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu Bara ambao unatarajiwa kuanza mwezi Agosti tarehe 26 mwaka huu.

Katika kipindi cha kwanza Simba ilionekana kutawala mpira vizuri na kupata goli la kuongoza katika dakika ya 33 ya mchezo ambapo Erasto Nyoni alifanikiwa kufumania nyavu za Bidvest na kufanya Simba kuongoza kwa goli moja mpaka wanakwenda katika kipindi cha mapumziko.

Kipindi cha pili kilipoanza timu ya Simba ilifanya mabadiliko makubwa ya kikosi chake kwa kuwatoa nje wachezaji wanne ambao ni Mzamiru Yassin, Jamal Mnyate, Salim Mbonde na Jamali Mwambeleko na kuwaingiza wachezaji Jonas Mkude, Mwinyi Kazimoto, Bakaba Paul na Ally Shomari.

Vikosi vyote vilionekana kuwa imara na kuzidi kupamba mpaka katika dakika ya 70 ya mchezo ambapo mchezajiwa wa klabu ya Bidvest aliweza kuzifumania nyavu za Simba na kusawazisha goli. Mpaka mpira unakwisha timu zote zilishindwa kuona lango la mwenzake na kutoka na sare ya goli 1-1.

Weka maoni