Everton waibuka na ushindi dhidi ya Gor Mahia katika ardhi ya Tanzania..

162

Tarehe 13.07.2017 itabaki kuwa ni historia katika nchi ya Tanzania ambapo klabu ya soka Ya Everton kutoka nchini Uingereza kwa mara ya kwanza ilitua nchini Tanzania kumenyana na Gor Mahia ambao ni washindi wa Michuano ya Sport Pesa Super Cup iliyokuwa imeandaliwa kwa udhamini mkubwa kwa Kampuni ya Ubetishaji ya Sport Pesa. Mchezo huu ulipigwa katika uwanja wa Taifa Jijini Dar Es Salaam ambapo wapenzi na mashabiki mbali mbali kutoka kila sehemu ya Tanzania na wengine kutoka nje ya Tanzania kuja kushuhudia mchezo huo ambapo kimsingi uligusa hisia za mashabiki wengi.

Mpira ulianza vizuri huku vilabu vyote vikicheza kwa tahadhali huku Everton wakionekana kuumudu mchezo kutokana na Gor Mahia kuonesha hofu mwanzoni mwa mchezo na kutokujiamini. Ilimchukua dakika 35 pekee Mshambuliaji wa Everton Wayne Rooney kuipatia Everton goli la kuongoza. Ikumbukwe

Wayne Rooney ni mchezaji aliesajiliwa kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Manchester United. Wayne Rooney ameanza maisha yake mapya ndani ya klabu hiyo kwa kishindo baada ya kutupia goli la kwanza ndani ya klabu hiyo tangia ajiunge wiki iliyopita akitokea Manchester United.

Baada ya dakika mbili tu mnamo dakika ya 37 mchezaji hatari huyu Tuyisenge Jacquer wa Gor Mahia alifanikiwa kuisawazishia Gor Mahia mpaka mpira unaenda Mapumziko Everton 1 Vs Gor Mahia 1. Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kujiamini ila ilipotimu dakika ya 77 Dowell akaipatia Everton goli la Pili na Mpaka dakika 90 za mchezo zinakamilika Licha ya kupambana kwa kasi, Mabingwa wa SportPesa Super Cup 2017, Gor Mahia waliishia kupigwa goli 2-1 dhidi ya Everton.

 

Weka maoni