Filamu ya ‘KIUMENI’ yatwaa tuzo tamasha la ZIFF.

184

Filamu ya ‘Kiumeni’ imeendelea kujizolea sifa kila kukicha.

Filamu hiyo ambayo imewakutanisha wastaa wa Bongo kama Idris Sultan, Ernest Napoleon, Muhogo Mchungu, Antu Mandoza, Rashid Matumla na wengine, imetikisa katika tuzo za tamasha la ZIFF linaloendelea huko visiwani Zanzibar kwa kufanya watu walioshiriki kuiandaa kunyakuwa tuzo mbili tofauti.

Tuzo ambazo zimenyakuliwa kupitia filamu ya ‘Kiumeni’ ni muongozaji bora wa filamu, ambaye ameshinda Nicholas Marwa na muandishi bora wa script, ambaye Daniel Manege ameshinda tuzo hiyo kupitia filamu hiyo hiyo.

Wengine walioshinda tuzo hizo za ZIFF ni Ibrahim Osward aliyeshinda tuzo ya muigizaji bora wa kiume, tuzo ya mpiga picha bora na editor bkra imekwenda kwa Kwetu Studio.

Tuzo ya muigizaji bora wa kike imekwenda kwa Hawa aliyetokea kwenye filamu ya T Junction na tuzo ya filamu bora kutoka Tanzania imekwenda kwa T Junction.

Weka maoni