Frankay arudi kwenye muziki na ngoma mbili baada ya kimya kirefu

363
Frankay

Msanii wa RnB na Afrobeat kutoka nchini Rwanda Kayiranga François ‘Frankay’ amerudi kwenye muziki baada ya kimya cha miaka miwili.

Leo hii (Jumapili) ametuletea ngoma mbili ambazo ni pamoja na Usichoke na Ngirira Vuba.

Anajitambulisha kama msanii ambaye ana nyimbo 10 ikiwemo tano ambazo hazijatoka kwani bado anaziongezea ubora studioni.

“Ilifika kipindi wazazi wakanikataza kufanya muziki kwa kuwa waliona nimepunguza kasi kwenye masomo halafu elimu ndio kitu cha kwanza katika ulimwengu wa leo, wakaniambia kwanza nisome nihitimishe elimu ya sekondari muziki nikaweka kando, ilikuwa mwaka 2014, mwaka mmoja baadaye ndipo nikamaliza elimu ya sekondari huko Musanze (Mkoa wa Kaskazini), baada ya hapo ndipo nikasema ngoja nijipange nirudi kwenye muziki na leo nimetoa nyimbo hizo mbili ambazo naamini zitafanya vizuri,” amesem Frankay katika mahojiano na Habari Pevu.

Frankay aliingia kwenye gemu la muziki mnamo mwaka 2010 ambapo alikuja na kibao chake cha ‘Ku bwanjye oya’ ambacho ndicho kilichomtangaza zaidi.

Pamoja na kwamba huu ni mwaka wa saba tangu aingie kwenye ramani ya muziki, anakiri kuwa jina lake bado halijawa kubwa kutokana na changamoto zinazowakabili wasanii ambao hawajawa na uwezo wa kipesa.

“Wasanii chipukizi tunakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo kualikwa kwenye matamasha kwani tunashindana na wasanii ambao wana majina makubwa hata nauli ya kuenda kuonana na mtangazaji saa zingine haipatikani, ila naamini nyota yangu itang’ara, nimeshaingia mkataba na lebo ya T-Time Pro na kuna vitu vingi tena vizuri wameniahidi,” ameongeza Frankay.

Frankay alizaliwa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo mwaka 1992.

Weka maoni