Gareth Bale awakosa Atletico Madrid

208

Mshambuliaji tegemeo wa timu ya Real Madrid, Gareth Bale atakosa mechi za nusu fainali za Ligi ya Mabingwa dhidi ya Atletico Madrid kutokana na tatizo la kigimbi cha mguu

Bale alitolewa alishindwa kuendelea na pambano la El Clasico na sasa imeripotiwa  anatarajiwa kuwa nje ya uwanja kwa wiki tatu.

Taarifa ya klabu ya Real Madrid kupitia katika tovuti yao inasema nyota huyo wa Wales amegundulika kuwa na tatizo la kigimbi cha mguu wa kushoto.

Wazo moja

  1. Thank you for this website but kindly tell us how we can learn Swahili. I can read and understand but I can’t speak. Habari Pevu mutusaidie

Weka maoni