Hawa ndio wagombea urais walioidhinishwa Rwanda

513

Leo Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini Rwanda imetangaza orodha ya wagombea urais walioidhinishwa.

Wagombea hao ni watatu kati ya sita walioonesha nia ya kuliongoza taifa la Rwanda kwa mhula wa miaka saba ijayo.

Walioruhusiwa kugombea urais ni pamoja na Paul Kagame, Frank Habineza wa chama cha Democratic Green Party of Rwanda na Philippe Mpayimana ambaye ni mgombea binafsi.

Rais Kagame kugombea urais kusaka awamu ya tatu baada ya katiba ya nchi hii kurekebishwa mwaka 2015
Kiongozi na mwasisi wa Chama cha Democratic Green Party of Rwanda, Frank Habineza
Philippe Mpayimana

Wengine ambao ni Diane Rwigara, Gilbert Mwenedata na Fred Barafinda, Rais wa NEC Profesa Kalisa Mbanda amesema hawajakidhi vigezo.

Diane Rwigara ameanza kuikosoa serikali baada ya baba yake kufariki dunia katika mazingira ya kutatanisha mwaka 2015
Fred Sekikubo Barafinda
Bwana Gilbert Mwenedata

Uchaguzi mkuu wa urais utafanyika tarehe 3-4 Agosti mwaka huu.

Rais Kagame ambaye anatarajiwa kupata ushindi, amekuwa madarakani tangu mwaka 2000.

Weka maoni