IGP Gasana awaasa watumia barabara kuwa makini kuelekea uchaguzi wa rais

178
Kamishna Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Rwanda, Gasana Emmanuel

Kamishna Mkuu wa Polisi nchini Rwanda (IGP) Emmanuel K. Gasana anawahamasisha Polisi katika kitengo usalama wa barabarani kuwa makini na kujiaanda katika kudhibiti ajali za mara kwa mara hususani katika nyakati hizi za kampeni ya uchaguzi wa rais.

Haya IGP Gasana ameyataja katika mkutano uliomjumuisha na askari polisi wa kitengo cha ulinzi wa barabarani wapatao 700.

Ameongeza kuwa juhudi zilizotumiwa katika kupunguza ajali za magari ambazo zilikuwa zikijitokeza inatokana na uhodari wa Polisi walio nao.

Aidha IGP Gasana amesema kuwa katika siku hizi za kampeni ya uchaguzi mkuu wa rais polisi wanapaswa kuweka jitihada kwani kutakuwa na safari nyingi ya magari katika shughuli za kampeni.

Imebainika kuwa ajali nyingi husababishwa na mwendo wa kasi unaotumiwa na madreva wa magari pia na kutotii amri na sheria za barabara vilevile na kutumia simu wakiwa wanaendesha gari.

Katika harakati za kupambana na ajali ya barabarani jeshi la polisi limechukuwa mikakati thabiti ikiwemo kuweka chombo kinachopunguza kasi ya gari kwa kila gari linalobeba abiria.

Weka maoni