Iradukunda Elsa kuipeperusha bendera ya Rwanda Miss World 2017

378

Miss Rwanda 2017 Iradukunda Elsa ndiye atakayeiwakilisha Rwanda kwenye mashindano ya urembo duniani yatakayowakutanisha nchini Uchina walimbwende kutoka mabara yote.

Kinyang’anyiro hicho cha Miss World 2017 kinakwenda kufanyikwa kwa mara ya 67 kwani mara ya kwanza ilikuwa mnamo mwaka 2051.

Inatarajiwa kuwa kitadumu kwa muda wa wiki tatu ambapo kitafanyika katika miji mbalimbali ya nchi ya Uchina.

Sherehe za kukunja jamvi na kutoa tuzo kwa washindi zitafanyika Novemba 18, 2017 mjini Shenzhen baada ya wasichana 130 watakaoshiriki shindano hilo kumenyana.

Taji la urembo la Miss World 2016 lipo mikononi mwa Stephanie Del Valle ambaye ni raia wa Puerto Rica.

Mrembo Stephanie Del Valle baada ya kuvishwa taji la mrembo namba mosi duniani katika sherehe zilizofanyika mjini Washindgton, D.C.

Miss Rwanda 2016 Mutesi Jolly ndiye aliwakilisha Rwanda kwenye shindano hilo la mwaka jana ambapo hakuweza kutwaa taji hata moja.

Mutesi Jolly, Miss Rwanda 2016

 

Weka maoni