Jay C awakemea marapa mateja ‘wanaokuwa kama sabuni’

348

Baada ya miezi mingi bila kutoa wimbo mpya, Rapa Jay C kutoka nchini Rwanda amerudi na wimbo wa ‘I am back’ aliomshirikisha Bruce Melody.

Katika mahojiano na Habari Pevu, Jay C amesema ameamua kurudi kwenye ulingo wa muziki ili kuuokoa muziki wa rap ambao umeshuka hadhi kupita kiasi kutokana na wasanii wa rap kutotoa ngoma za maana huku wengine wakijiingiza katika janga la madawa ya kulevya.

Amesema alikuwa amejitenga kidogo na muziki ili aweze kuitunza familia yake, lakini leo amerudi na anataka watu watambue utamu wa rap.

“Unajua nina mke na watoto wawili, nilikuwa nimejiweka kando ili niweze kuwashughulikia vizuri ila sasa nimerudi rasmi, muziki wa rap ulishuka hadhi tangu niondoke, wapo marapa ambao wametoweka kwenye sanaa za muziki na wengine ambao bado wapo ila hawana jipya, kwa hiyo nimeamua kurudi ili niwape uhondo wapenzi wa rap.”

“Hata raia wa kawaida hutumia madawa ya kulevya siyo wasanii tu wanatumia, ila baadhi ya wasanii hutumia madawa hayo wakiamini kuwa yatawapa inspiration na kuwaweka kwenye mood nzuri wakati si kweli, halafu leo yapo madawa ya kulevya yanayoitwa Mugo (heroine) ambayo madhara yake ni zaidi ya madhara ya bangi…” ameongeza Jay C.

Katika wimbo wake huo wa I am back, Jay C anawachana pia wasanii wanaotumia umaarufu wao mashabiki wao wa kike kwa kufanya nao ngono, ambapo wengine huwabebesha mimba watoto hao na kuwatelekeza.

Amesema ukosefu wa maadili mema kwa baadhi ya marapa ndio husababisha muziki wa rap usipate maendeleo, ambapo amewataja wasanii hao kuwa wanakuwa kama sabuni.

Jay C ambaye majina yake halisi ni Muhire Jean Claude, ni miongoni mwa nguzo mahiri za muziki wa rap nchini Rwanda.

Amekuwa kwenye gemu tangu mwaka 2006ambapo ndipo aliachia wimbo wake wa kwanza.

Wazo moja

  1. Huyu jamaa ana flow nzuri sema sijui anaimba kilugha gani, nimeambiwa kinyarwanda na kiswahili ni lugha zenye ukaribiano mkubwa wa kimaneno ila sijaambulia hata neno moja, wadau niambie anaimba nini maana dah Kinyarwanda noma aisee

Weka maoni