Joseph Kabila: Sijawahi kuahidi kuandaa uchaguzi DR Congo

360
Rais wa DR Congo Joseph Kabila

Rais wa Jamhuri ya Kidemokradia ya Congo, Joseph Kabila Kabange amesema hajawahi kuahidi kuandaa Uchaguzi Mkuu nchini nchini mwake mwaka huu.

Kabila ameliambia Jarida la kila wiki la Ujerumani la Der Spiegel kuwa hajaahidi chochote lakini anapenda Uchaguzi ufanyike haraka iwezekanavyo.

Aidha, amesema anataka uchaguzi mzuri lakini sio tu kufanya uchaguzi, kwa mujibu wa RFI.

Hayo yanajiri wakati ambapo joto la kisiasa kuhusu uchaguzi kufanyika mwaka huu nchini DR Congo limeendelea kupanda, huku upinzani hasa ule unaoongozwa na mwana wa aliyekuwa kiongozi wa kihistoria wa upinzani Etienne Tshisekedi ukiendelea kugawanyika.

Hivi karibuni muungano huo wa Rassemblement uligawanyika baada ya uteuzi wa Waziri Mkuu kutoka muungano huo Bruno Tshibala.

Hali ya kisiasa nchini Dr Congo inaendelea kutisha , huko watu wengi wakiendelea kukamatwa na wengine kuuawa.

Wiki iliopita Umoja wa Ulaya na Marekani waliwachukulia vikwazo maafisa kadhaa wa serikali ya DRC kwa kuchochea uhasama na kuchangia kushindwa kuandaa uchaguzi mwaka huu.

Wazo moja

  1. Rais huyu amekuwa madarakani kwa miaka mingi si aachie madaraka na wengine waongoze? Ndo kitu ambacho kinawaponza waafrika akifika madarakani hataki kutoka hapo sasa ndo waasi wanaanza kumvizia

Weka maoni