Kagame aipongeza Kenya kwa ujenzi wa reli Nairobi-Mombasa

511
Reli mpya ya kuunganisha Mombasa na Nairobi inatarajiwa kusaidia klupunguza muda na gharama ya usafirishaji wa bidhaa (Picha/CNBC Africa)

Rais Kagame ameisifia Kenya kwa kuingia enzi mpya katika sekta ya uchukuzi ambapo nchi hiyo imezindua reli ya kisasa kutoka bandari ya Mombasa kwenda jijini Nairobi.

Reli hiyo ilijengwa kwa udhamini wa Serikali ya Uchina. Rais Uhuru Kenyatta ndiye aliyeongoza shughuli ya uzinduzi wake hapo jana Jumatano.

Reli mpya ya Kenya ambayo imejengwa kwa udhamini na usimamizi wa serikali ya Uchina

Reli hiyo inatarajiwa kupunguza muda wa kusafirisha bidhaa kutoka bandarini Mombasa hadi mataifa mengine ya Afrika Mashariki.

Akizindua ujenzi wa reli hiyo mwaka 2013, Rais Kenyatta alisema mataifa ya Kenya, Uganda na Rwanda yalikubaliana kustawisha maendeleo kwa kujenga reli ya kisasa kuunganisha Mombasa, Kampala na Kigali, kwa mujibu wa Swahili Hub.

Safari ya kutoka Mombasa kuelekea Nairobi na treni ya kisasa itachukua saa nne na nusu ikilinganishwa na saa tisa kwa kutumia basi na saa 12 kwa kutumia treni ya zamani.

Nauli ya watu watakaokalia viti vya kawaida ni shilingi 900 huku wale watakaosafiri kwa kutumia business class wakilipa shilingi 3,000.

Reli hiyo iliotengezwa kupitia ufadhili wa shilingi bilioni 3.2 kutoka serikali ya China ndio mradi mkubwa wa miundo msingi kuwahi kutekelezwa na serikali tangu taifa hilo lijipatie uhuru wake, kwa mujibu wa BBC.

Gharama ya mradi huo imekosolewa na upinzani ambao unasema mradi huo umeigharimu Kenya fedha nyingi mno.

Vilevile wamemshutumu rais Kenyatta kwa kuomba fedha kutoka China bila mpango.

Serikali nayo inasema kuwa ni sharti iwekeze katika miundo msingi ili kuvutia wawekezaji.

Katika hatua nyingine Rais Kenyatta amesema atakayehujumu usalama wa reli hiyo atakabiliwa na adhabu kali ikiwemo hata kunyongwa kama itabidi.

Wazo moja

  1. Kenya ni mfano wa kuigwa kwa mataifa ya Afrika Mashariki. Inajitahidi sana kukuza uchumi wake na nadhani uchumi wake ndo unaongoza kwa Afrika Mashariki. Ahsante sana Rais Kagema kwa ujumbe wako wa pongezi na endelea kukuza urafiki baina ya Rwanda na Kenya pamoja sana

Weka maoni