Kelechi Iheanacho njiani kuhamia Leicester City

108

Kelechi Iheanacho amekamilisha vipimo vya afya na klabu ya Leicester City na yuko tayari kukamilisha uhamisho wake kutoka katika klabu ya Manchester City, kwa mujibu wa ripoti mbalimbali.

Ripoti hizo zinadai kwamba Iheanacho na Leicester wamefikia makubaliano na uhamisho huo wa ada ya paundi milioni 25 unakaribia kumalizika.

Timu ya Manchester City wanaamini kwamba mchezaji huyo Mnigeria, mwenye umri wa miaka 20, ana uwezo wa kuwa mmoja wa wafungaji bora duniani lakini klabu hiyo inapata shida na sehemu ya kumpa Iheanacho ili aweze kucheza kwenye kikosi cha kwanza.

Weka maoni