Kenyatta amshukuru Kagame, amualika kutembelea Madaraka Express

466
Rais Kagame akipokelewa na mwenyeji wake Kenyatta alipotembelea Kenya, Januari 2014. (Picha/Urugwiro Village)

Baada ya rais wa Rwanda, Paul Kagame kuisifia Kenya kwa kujipatia reli ya kisasa, rais wa nchi hiyo Uhuru Kenyatta amemshukuru na kumualika kutembelea treni hiyo.

Reli hiyo iliyobatizwa jina la Madaraka Express ina urefu wa kilomita 472 ambapo treni zinasafiri kwa kasi ya wastani ya kilomita 120 kwa saa.

Rais Kagame mwishoni mwa mwezi jana baada ya reli hiyo kuzinduliwa, aliitumia Kenya ujumbe wa pongezi.

Kagame aipongeza Kenya kwa ujenzi wa reli Nairobi-Mombasa

Akijibu ujumbe huo, Rais Kenyatta amemshukuru Rais Kagame kwa ujumbe wake na kumualika kutembelea reli hiyo ya Madaraka Express ambayo imeanza kutumiwa.

Rais Kenyatta amegusia pia suala la mahusiano baina ya nchi hizo mbili, akisema Rwanda na Kenya zimekuwa na mahusiano ya kuridhisha na kumuomba Mungu aendelee kuneemesha mahusiano hayo.

Reli hiyo iliyojengwa kwa udhamini wa Serikali ya Uchina, inatarajiwa kupunguza muda wa kusafirisha bidhaa kutoka bandarini Mombasa hadi mataifa mengine ya Afrika Mashariki.

Safari ya kutoka Mombasa kuelekea Nairobi na treni ya kisasa itachukua saa nne na nusu ikilinganishwa na saa tisa kwa kutumia basi na saa 12 kwa kutumia treni ya zamani.

Wazo moja

  1. Rwanda na Tanzania ni ndugu, nawapenda sana Wanyarwanda, nawaombea marais wetu waendelee kupendana na wenyewe kwa ajili ya kizazi kijacho. We have much in common

Weka maoni