Kesi ya Wema hatima yake kujulikana Agosti Nne

118

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeahirisha kesi ya dawa za kulevya inayomkabili muigizaji  Wema Sepetu hadi Agosti 4/2017 kwa ajili ya kutoa uamuzi wa kupokea au kutopokea vielelezo vya ushahidi wa sampuli ya mkojo na bangi.

Hatua hiyo inatokana na Wakili wa Wema Sepetu na wenzake, Peter Kibatala kumuomba Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kutopokea vielelezo vya ushahidi huo kutoka kwa Mkemia wa Ofisi ya Mkemia Mkuu Dar es Saalam,  Elias Malima.

Katika ushahidi wake, Malima ameeleza kwamba mwezi wa pili tarehe  6/2017 alipokea sampuli ya majani ya bangi na  tarehe 8 ya mwezi wa pili alipokea tena sampuli ya mkojo wa msanii Wema Sepetu.

Wakili wa serikali Constantine Kakolaki aliiomba mahakama ipokee vielelezo vya ushahidi huo, hata hivyo wakili Kibatala alipinga kwa madai ripoti haijakidhi vigezo.

Kutokana na mvutano wa kisheria Hakimu Simba ameahirisha kesi hiyo hadi  tarehe 4 mwezi Agosti mwaka huu.

Weka maoni