Kitoko Bibarwa kutua Rwanda leo kumuunga mkono Rais Kagame

212

Msanii wa miondoko ya Afrobeat Kitoko Bibarwa anatarajiwa kuwasili uwanja wa ndege wa Kigali usiku wa leo Jumatano kutoka masomoni nchini Uingereza.

Hitmaker wa ‘Rurashonga’, ‘Agakecuru’, Amadayimoni’, ‘Ikiragi’ ‘Urankunda bikandenga’, ameamua kurudi nchini mwake ili kuwatumbuiza watakaojitokeza kwa ajili ya kampeni za Rais Kagame.

Uchaguzi mkuu wa urais ambao rais Paul Kagame anatarajiwa kugombea utafanyika tarehe 3-4 Agosti 2017 na msanii Kitoko Bibarwa amealikwa kwenye shughuli hizo.

Itakuwa si mara ya kwanza kwa Kitoko kuunga mkono kampeni za urais za Rais Kagame, kwani hata mwaka 2010 alifanya hivyo pamoja na wasanii wenzake kama Tom Close, Tuyisenge, Senderi na King James.

Kampeni za urais zitaanza mnamo tarehe 14 Julai, kwa mujibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Weka maoni