Klabu ya Simba sasa kuweka kambi Afrika ya Kusini

551

Katika harakati za kujiandaa kwa msimu mpya klabu ya Simba SC ambao ni Mabingwa wa Kombe la FA, Wanatarajia kuondoka nchini kesho kutwa Jumanne kwenda Afrika Kusini kwa maandalizi ya msimu mpya ujao.

Taarifa iliyotolewa na Idara ya Habari na Mawasiliano ya klabu hiyo, imesema Simba SC ikiwa Afrika Kusini itacheza mechi za kujipima nguvu na timu za huko ili Mwalimu aweze kuona mapungufu na kuyafanyia kazi kabla ya msimu mpya kuanza.

Klabu ya Simba itarejea siku chache kabla ya Tamasha lao kubwa la kila mwaka la Simba Day siku ya Tarehe 08/08/2017, ambapo kutakuwa na mechi ya kimataifa, sherehe ambazo zitaambatana na utambulisho wa jezi yao mpya itakayotumiwa msimu ujao.

Weka maoni