Knowless kumenyana na Victoria Kimani, Vanessa Mdee tuzo za NEA 2017

330

Malkia wa muziki wa Rwanda Butera Knowless ametajwa kuwania tuzo za Nigerian Entertainment Awards 2017.

Anatarajiwa kusaka tuzo kwenye kipengele cha msanii bora wa Afrika ukitoa wasanii wa Nigeria.

Atamenyana na wasanii wenye hadhi kubwa kwenye muziki kama Amanda Black wa Afrika Kusini, Victoria Kimani wa Kenya, Vanessa Mdee wa Tanzania, Sheebah Karungi wa Uganda Efya wa Ghana na  Queen Vee kutoka Zimbabwe.

Knowless

Siku zinavyozidi kusonga mbele ndivyo nyimbo za Butera Jeanne d’Arc almaarufu Knowless ikiwemo Ujumbe, Te amo, Ujya unkumbura zinavyovivutia vituo vya runinga vya kimataifa.

 

Kupitia mtandao wa Instagram, mwanamke huyu ambaye ana mume na mtoto mmoja amedai kufurahishwa na kutajwa kuwania tuzo hizo katika kipengele cha Best Africa Female Artist [Non-Nigerian).

Tuzo za NEA zilianza kutolewa mwaka 2006 kwa malengo ya kuwasania wasanii mbalimbali ikiwemo wanamuziki, waigizaji wa watayarishaji wa filamu.

Weka maoni