Macron awa rais mdogo Ufaransa baada ya Napoleon Bonaparte

419
Rais mteule wa Ufaransa Emmanuel Macro

Baada ya kutoana kijasho, hatimaye Emmanuel Macron amempiga chini Marine Le Pen kwa kupata asilimia 65 ya kura katika duru ya pili ya uchaguzi.

Akiwa na umri wa miaka 39, Emmanuel Macron anakuwa rais mdogo katika historia ya Ufaransa baada ya Napoleon Bonaparte aliyeingia madarakani akiwa na miaka 30.

Baada ya kuvishwa cheo cha Jenerali jeshini akiwa ni kijana wa miaka 24, Napoleon Bonaparte uongozi wa taifa la Ufaransa mnamo mwaka 1799.

Katika kampeni zake, Bw Macron ameahidi kuhakikisha Ufaransa inaendelea kuwa sehemu ya Umoja wa Ulaya ambao ni mwanzilishi, tofauti la Marine le Pen aliyelenga kuwatoa Wafaransa katika umoja huo.

Aidha, Macro kutoka chama cha En Marche! alichoasisi mwaka jana, anakuwa rais wa kwanza kuchaguliwa kutoka nje ya vyama viwili vikubwa nchini humo.

Baada ya matokeo ya uchaguzi kutangazwa, Macron amesema umefunguka ukurasa mpya katika historia ya Ufaransa, na ameahidi kupigania umoja miongoni mwa wananchi.

Alishikilia wadhifa wa waziri wa uchumi kwa muda ya miaka miwili kabla ya kujiuzulu, ila hii ndiyo mara yake ya kwanza kuingia mamlakani kupitia njia ya uchaguzi.

Baada ya kutonyookewa na mambo, Marine le Pen amemtumia Macron ujumbe wa kumpongeza, akisema lazima ampongeze ingawaje anasubiriwa na changamoto nyingi.

Marine Le Pen

Endapo hatamuoa mke mwingine au kumpata mtoto nje ya ndoa, Emmanuel Macron atakufa bila kuacha mtoto kwani kufikia sasa hana mtoto hata mmoja.

Alioana na Brigitte Trogneux miaka 10 iliyopita ambapo mke huyo kwa sasa ana umri wa miaka 64.

Inadaiwa mahusiano yao yalianza wakati Brigitte alipokuwa mwalimu wake wa Kifaransa kipindi anasomea elimu ya sekondari.

Macro na Brigitte

Brigitte ana watoto 3 aliozaa na André-Louis Auzière kabla ya ndoa yao ya miaka 32 kuvunjika ikiwa ni mwaka 2006.

Weka maoni