Magufuli ajivunia kutumia mitandao yote ya simu

360
Rais Magufuli leo (Picha/Nipashe)

Rais wa Tanzania, Dkt John Joseph Pombe Magufuli, amesema anajivunia kuwa ana mitandao mingi ya simu ambayo inamsaidia kuwasiliana bila kero wakati wowote.

Amesema hayo leo Juni Mosi, wakati wa uzinduzi wa mfumo wa ulipaji kodi kwa njia ya elektroniki.

“Mimi nina mitandao yote ya simu, nina Tigo, Airtel, Vodacom na hata TTCL, mtu akinitafuta huku Airtel akanikosa ninaweza kuweka Tigo, ili mradi ninatambulika kila mahali,” amesema.

Pia amesema mitandao yote ya simu inamsaidia kupata taarifa mbalimbali zinazoendelea nchini Tanzania na duniani, kwa mujibu wa Mwananchi.

Hata hivyo, Rais Magufuli amezitaka kampuni za simu kuhakikisha zinalipa kodi ili serikali isikose mapato yake.

“Watu hawakupenda kulipa kodi hata kipindi cha Yesu hawakutaka hadi walipoambiwa ya Kaizari mpeni Kaizari,” ameongeza Rais Magufuli, kwa mujibu wa Nipashe.

Wazo moja

  1. Naskia marais wengine wanatumia simu zenye mifumo ya satelite sasa yeye kwa nini anaendelea kutumia hiyo mitandao duni? Matapeli wa mitandao watamvamia nakuapia

Weka maoni