Makamuzi ya Charly na Nina ndani ya Rwanda Fiesta

264
Charly na Nina wakiimba wimbo wao wa Owooma waliomshirikisha Geo Steady wa Uganda

Wanadada Charly na Nina wanaounda kundi la muziki la ‘Charly na Nina’ kutoka nchini Rwanda ni miongoni mwa wasanii waliokuwepo kwenye tamasha la Rwanda Fiesta lililofanyika wikiendi iliyopita.

Ni tamasha la kihistoria ambalo wasanii kama Morgan Heritage kutoka Jamaica na Diamond kutoka Tanzania walikuwa wamealikwa kuirutubisha mioyo ya Wanyarwanda.

Charly akiwa jukwaani

Tamasha hilo lililoandaliwa na Clouds TV Rwanda lilifanyika maeneo ya Nyamata wilayani Bugesera katika Jimbo la Kusini, ambapo kulikuwa na utitiri wa wadau wa muziki.

Mashabiki walionekana wamezikariri nyimbo za Charly na Nina

Ukiacha Morgan Heritage na Diamond Platnumz, walikuwepo hata Chege Chigunda na Vanessa Mdee kutoka Tanzania, na Yvan Buravan na Dj Pius kutoka nchini Rwanda.

Nina na madensa wao wawili wakikamua stejini

Diamond alivyokiwasha Rwanda Fiesta, wasichana wapagawa (Picha+Video)

Weka maoni