Mama yake na Zari mgonjwa taabani

Mama yake na Zari mgonjwa taabani

1440
Familia ya msanii Diamond Platnumz na mkewe Zari The Boss Lady ipo kwenye wakati mgumu baada ya mama yake na Zari kuwahishwa hospitali kwa matibabu.

Magazeti ya Uganda yamemnukuu Zari akisema mama yake mzazi anaumia sana na kuwataka mashabiki wake wamkumbuke kwenye ibada zao.

“Mama yangu yupo hospitali anaugua sana. Naomba mmuombee sana iwezekanavyo yafadhali. Ahsanteni,” amesema Zari.

Tuwakumbushe kwamba siku za nyuma pia mzazi huyu alikuwa mahtuti hospitalini, ambapo alirudishwa nyumbani baada ya kupata ahueni.

Zari alifiwa na mume Ivan Semwanga, baba wa watoto wake wa tatu wa kwanza.

Kaburi la Ivan Semwanga kufukuliwa? Mrundo wa pesa alizozikwa nazo zimezua utata

 

Weka maoni