Mani Martin ammiminia sifa Eddy Kenzo akielezea Afro Remix

260
Mani Martin na Eddy Kenzo

Mani Martin amemmwagia sifa kibao nguli wa muziki wa Uganda Eddy Kenzo baada ya wawili hao kushirikiana katika remix ya wimbo Afro wa Mani Martin unaofanya vizuri nchini Rwanda.

Kwa mtazamo wa Mani Martin, “Eddy Kenzo si msanii wa Uganda tu ama wa Afrika Mashariki, ni msanii ambaye amejitahidi kuwakilisha muziki wake Afrika nzima.”

Ameongeza, “unajua alitwaa BET Award na AFRIMA Award pia, kwangu ni msanii ambaye anafanya vizuri kwa African Music Revolution and that’s really inspire me a lot.”

Juzijuzi Mani Martin alikuwa nchini Uganda ambapo kwa uungaji mkono wa Eddy Kenzo walifua dafu kurekodi Afro Remix na amesema wimbo huo unakaribia kumalizika.

Eddy Kenzo ni msanii mkubwa nchini Uganda ambaye ana jina ambalo si dogo nchini Rwanda. Miaka miwili iliyopita alifunguka kuhusu asili yake na kusema kuwa mama yake mzazi ni Mnyarwanda.

Mani Martin ni miongoni mwa wasanii mahiri nchini Rwanda ambao wanafanya muziki wa miondoko ya Afro Beat.

Amesema aliamua kumshirikisha Eddy Kenzo kwa sababu hata Eddy Kenzo katika uimbaji wake huvipa kipaumbele vionjo vya asili vinavyoonyesha utamu wa muziki wa Afrika.

Katika mahojiano na Habari Pevu, Mani Martin amesema “niliwazia kufanya remix ya Afro na msanii ambaye anajulikana barani Afrika tangu niliporelease the original one, lakini sasa Eddy Kenzo akawa wa kwanza kwa kumfikiria kwa sababu yeye ni msanii ambaye anatumia sana african danses nikawa na bahati nay eye mwenyewe akapenda wimbo, nilipomuambia tufanye remix akakubali bila kusita”

Amewataka mashabiki wake wakae mkao wa kula kwani wimbo wenyewe umepelekwa nchini Afrika Kusini  kwa ajili ya umaliziaji (mastering) ambapo ukimalizika utaingia mitandaoni tayari kusikilizwa.

“Wimbo kama umeshamalizika sema mastering ndio bado inashughulikiwa huko Afrika Kusini, ni wimbo mzuri ambao naamini wapenzi wa muziki wangu wataupenda.”

Iangalie Afro Original

Weka maoni