Mani Martin feat. Eddy Kenzo – Afro Remix

226
Cover ya remix ya Afro, wimbo ambao Mani Martin kamshirikisha Eddy Kenzo

Remix ya wimbo wa Afro wa Mani Martin ambayo amemshirikisha msanii kutoka Uganda Eddy Kenzo hatimaye imetoka.

Imetengenezwa na maproduza wawili ambao ni pamoja na Pastor P (Rwanda) na Kuseim (Uganda).

Kwa mujibu wa Mani Martin katika mahojiano na Habari Pevu, hata video yake imeshatengenezwa ila produza Meddy Saleh (Rwanda) bado anaifanyia umaliziaji.

Ila kwa nini Mani Martin akaamua kufanya remix ya wimbo wake huo na kumshirikisha Eddy Kenzo? Amesema alifanya hivyo ili kutanua soko la muziki wake.

Kwa mtazamo wa Mani Martin, “Eddy Kenzo si msanii wa Uganda tu ama wa Afrika Mashariki, ni msanii ambaye amejitahidi kuwakilisha muziki wake Afrika nzima.”

Ameongeza, “unajua alitwaa BET Award na AFRIMA Award pia, kwangu ni msanii ambaye anafanya vizuri kwa African Music Revolution and that’s really inspire me a lot.”

Mani Martin ni miongoni mwa wasanii mahiri nchini Rwanda ambao wanafanya muziki wa miondoko ya Afro Beat.

Unaweza kuangalia video ya Afro Original hapa chini

Weka maoni