Marufuku mifuko ya plastiki yaanza kufanya kazi Kenya

139

Marufuku ya matumizi ya mifuko ya Plastiki nchini Kenya imeanza kutekelezwa  jana ambapo mtu yeyote atakayekutwa akiuza, kutengeneza au kuitumia mifuko hiyo atakabiliwa na faini ya Dola za Kimarekani elfu 38 ama kifungo cha hadi miaka minne jela.

Serikali imesema, marufuku hiyo itasaidia kulinda mazingira lakini watengenezaji wa mifuko hiyo wakidai uamuzi huo utaathiri ajira elfu 80 ambapo inasemekana Wakenya hutumia mifuko ya Plastiki milioni 24 kwa mwezi.

Uamuzi huo wa Kenya unaelezwa kuwa mgumu ambao umeshindwa kutekelezwa na nchi nyingi duniani. Nchi nyingine za Afrika zilizopiga marufuku matumizi ya mifuko ya Plastiki ni pamoja na Rwanda, Mauritania, na Eritrea.

Weka maoni