Mbunge wa Rwanda Mukayisenga Françoise afariki dunia

233
Marehemu Mukayisenga Françoise

Bunge la Rwanda limeondokewa na mbunge Mukayisenga Françoise aliyefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Jeshi la Ulinzi ya Kanombe mjini Kigali.

Taarifa ya bunge kuhusu kifo hicho inasema marehemu alikuwa anaumwa ila ugonjwa uliokuwa unamsumbua haukubainishwa.

Katika taarifa iliyotolewa kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter, Bunge la Rwanda limesema limesikitishwa sana na kifo cha mbunge husika.

Mukayisenga ameiaga dunia akiwa na umri wa miaka 48. Alipewa nafasi ya ubunge kwa tiketi ya chama tawala cha RPF-Inkotanyi kutoka Mkoa wa Magharibi.

Mwanamke huyo alikuwa na uzoefu mkubwa katika masuala ya uongozi ambapo alianza kufanya siasa mwaka 1992 akihudumu katika Wizara ya Fedha na Mipango.

 

 

Weka maoni