Mchezaji Douglas Costa amesajiliwa na Juventus.

135
Mabingwa wa soka nchini Italia,Juventus wamekiongezea makali kikosi chao tayari kwa msimu mpya wa Seria A baada ya leo kutangaza kumsajili winga wa kimataifa wa Brazil,Douglas Costa kwa mkopo wa msimu mmoja akitokea Bayern Munich ya Ujerumani.
Costa mwenye umri wa miaka 24 amejiunga na Juventus ikiwa ni muda mfupi tangu Bayern Munich itangaze kumsajili kiungo wa kimataifa wa Colombia,James Rodriguez kutoka Real Madrid ya Hispania kwa mkopo wa misimu miwili.
Aidha Juventus italazimika kuilipa Bayern Munich kiasi cha Euro Milioni 6 kama ada ya kumsajili Costa kwa mkopo huo wa msimu mmoja kisha italazimika kuongeza Euro Milioni 1 zaidi ikiwa atatwaa vikombe na klabu hiyo.
Wakati huohuo Juventus imepewa nafasi ya kumsajili moja kwa moja Costa mwishoni mwa msimu ujao kwa ada ya €40m itakayolipwa katika kipindi cha miaka miwili.
Costa alianzia soka lake kwenye klabu ya Gremio ya nyumbani kwao Brazil kabla ya Januari 2010 kujiunga na Shakhtar Donetsk ya Ukraine ambayo alidumu nayo kwa misimu mitano na kuhamia Bayern Munich Agosti 2015.
Akiwa na Bayern Munich, Costa kufanikiwa kufungia miamba hiyo ya Bavaria mabao 14 katika michezo 76.

Weka maoni