Mchezaji Lionel Messi aweka rekodi mpya La Liga

151

Mshambuliaji wa klabu ya Barcelona, Lionel Messi baada ya kufunga mabao mawili jana usiku dhidi ya klabu Alaves, ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kufikisha magoli 350 ligi kuu Hispania ‘La Liga’ .

Rekodi nyingine aliyoiweka ni kuwa mchezaji wa pili kufunga zaidi ya magoli 350 kwenye ligi kubwa tano barani Ulaya akiwa na timu moja nyuma ya mshambuliaji gwiji wa zamani wa klabu ya Bayern Munich, Gerd Muller mwenye magoli 365.
Kwa sasa, Messi amempita hasimu wake Ronaldo kwa magoli 66 ya ligi huku Ronaldo akiwa amecheza michezo michache ya ligi kuliko Messi.

Weka maoni